Kilimo bora cha pilipili kichaa (african birds-eye chili)



UTANGULIZI
Pilipili ni aina ya pilipili kali. Hustahimili hali ngumu ya 
kimazingira na hazina magonjwa na wadudu wengi. Hali hii hufanya gharama ya ukuzaji
kuwa chini zaidi kushinda mimea mingine. Pilipili kichaa ina wingi wa vitamin A na C na
hutumika kama kiungo kwa chakula. Pia inaweza kukaushwa.
HALI YA HEWA
Huvumilia hali nyingi ikiwemo; joto na ukame ukizingatia
unyunyizaji maji. Hata hivyo hali nzuri kwa mmea huu ni uvuguvugu na joto.
Pia inahitaji mvua ya kadri kati ya 600mm – 1200mm kwa mwaka.
Hali ya maji mengi mchangani hata kwa mda mchache husababisha kuanguka kwa majani.
Pia upande mwingine ukame husababisha kuanguka kwa maua kwa hivyo nyunyiza maji.
AINA YA UDONGO
Hufanya vizuri katika aina tofauti za udongo, lakini zingatia usiwe udongo wa kutuamisha maji.
Mmea huu hufanya vizuri unapotumia samadi.
MBEGU
Tumia mbegu iliyothibitishwa na kampuni ya MACE FOODS LTD. Nao kampuni hii
hununua hili zao.
KUTAYARISHA KITALU
Weka kitalu mita moja upana kwa urefu upendao kulingana na mbegu yako.
Elekeza kitalu chako upande ambao jua lisiunguze miche.
Piga mistari ya 10 cm na weka mbegu, funika udongo kidogo. Weka manyasi makavu na nyunyizia maji asubuhi na
jioni.
Zinapoanza kuota, ondoa nyasi na weka kivuli mita moja juu na endelea kunyunyizia maji.
KUPANDA
Panda kachachawa miche ikiwa na majani halisi manne. Itakuwa imefika wiki sita.
PALIZI
Palilia mara mbili kwa msimu kuapata mavuno mengi zaidi
Kwa mazao bora panda mmea huu pekee yake 1 meter x 1 meter. Lakini ukitaka unaweza kuchanganya na mmea mingine.
Weka samadi na baada ya wiki moja weka DAP kuongeza rutuba ya udongo. Pia weka CAN baada ya wiki tatu zaidi.
KUHIFADHI UNYEVU
Tandika manyasi makavu ili kuhifadhi unyevu na kuthibiti hali ya joto la udongo.
Tunashauri kuonana na wataalamu wa kilimo kwa ushauri zaid ili kilimo chako kiwe chenye tija zaidi.

Kilimo cha Bilinganya Nyeupe



Zao lenye pato kubwa
Bilinganya nyeupe (Long White Eggplant) ni moja ya zao la mbogamboga ambalo lina viini lishe vingi na muhimu kama vile madini aina ya chokaa na chuma, Vitamini A, B na C, wanga, protini na maji
Kisayansi zao hili hujulikana kama Solanum Melongenai na kilimo chake huweza kufanyika katika majira yote ya mwaka.
Hali ya Hewa
Zao hili huhitaji hali ya joto la wastani, udongo wenye kina kirefu na rutuba ya kutosha na usiotuamisha maji. Kwa kawaida bilinganya hulimwa zaidi ya msimu mmoja, lakini katika nchi za kitropiki (joto) zao hili hulimwa kwa msimu mmoja.
Udongo
Zao la hili huota katika udongo wa kichanga na tifutifu, wenye rutuba ya kutosha. Unashauriwa kuweka mboji katika shamba lako ili kuurutubisha udongo vizuri.
Utayarishaji wa kitalu na usiaji
Ni muhimu kusia mbegu katika trei ili kukwepa kupotea kwa miche pamoja na kupata miche bora. Miche huchukua siku saba hadi kumi kuchipuaa, na wiki tatu hadi nne kwenye kitalu, kisha kupelekwa shambani. Ikiwa mkulima atasia mbegu ardhini, ni vyema kuandaa eneo lenye mbolea ya kutosha. Waweza kuweka mbolea ya mboji katika eneo hilo au katika matuta yako uliyoyaandaa kwa ajili ya kusia mbegu.
Upandaji wa miche
Unapopeleka miche yako shambani, hakikisha unaotesha kwa kufuata maelezo muhimu ya utaalamu ili kuweza kupata mavuno mengi na yenye ubora. Matuta ya kunyanyua yasiyotuwamisha maji hushauriwa kutumika katika kilimo cha zao hili kwani huzuia kuoza kwa mimea maji yanapotuama. Nafasi kati ya mche na mche iwe sentimeta 60 huku nafasi kati ya mstari na mstari iwe ni hatua moja. Hakikisha shamba limemwagiliwa na weka mbolea ya mboji katika kila shimo wakati wa kuotesha.
Umwagiliaji
Zao hili likipata maji ya kutosha husitawi vizuri hivyo ni muhimu kumwagilia mara mbili hadi tatu kwa wingi kulingana na msimu husika hasa wakati wa kiangazi. Usimwagilie kipindi cha mvua kwani utasababisha bilinganya kuoza kutokana na wingi wa maji.
Palizi
Hakikisha unafanya palizi mara kwa mara na kuacha shamba likiwa safi wakati wote ili kuondoa ushindani wa magugu na mimea kwenye chakula, maji na mwanga. Pia kuzingatia usafi kutasaidia kupunguza kuzaliana kwa wadudu waharibifu pamoja na magonjwa.
Magonjwa na wadudu
Zao hili hushambuliwa na wadudu pamoja na magonjwa ya aina mbalimbali hasa linapolimwa wakati wa kiangazi.
Utitiri: 
Wadudu hawa kwa kiasi kikubwa wamekuwa visumbufu vya zao hili na si rahisi kukuta bilinganya haijashambuliwa na wadudu hawa, hasa wakati wa joto au kiangazi.
Kimamba: Hawa wadudu pia hushambulia bilinganya mara kwa mara wakati wa kiangazi.
Inzi weupe (white flies): 
Wadudu hawa kwasasa ni visumbufu vya mazao mengi ya bustani ama ya mbogamboga, na bilinganya ni moja ya mazao yanayoshambuliwa na wadudu hawa kwa kiasi kikubwa. Bilinganya inapoanza kuzaa matunda, wadudu hawa huvamia na hujikita katika majani, hufyonza maji na hatimaye bilinganya hukauka. Wadudu hawa hueneza ugonjwa unaofahamika kwa jina la Rasta. Huweza pia kusababisha majani kubadilika rangi na kuwa meusi
Barafu: 
Huu ndio ugonjwa mkubwa unaosumbua zao la bilinganya, na mara nyingi ugonjwa huu hutokea kipindi cha mvua. Husababisha tunda ya bilinganya kupata ukungu, kuoza na kudondoka kwenye mti. Na inaposhika tunda moja, ni rahisi kuambukiza lingine kwa haraka na matunda ya mti wote hushambuliwa. Pia wadudu kama leaf miner, bollworm, beetle pamoja na magonjwa kama root rot, leaves sports , kutu, kuoza kwa tunda, bakajani hushambulia zao hili pia.
Namna ya kudhibiti
Wadudu huweza kudhibitiwa kwa kutumia mwarobaini, tumbaku, majivu na mafuta ya taa, majani ya mustafeli pamoja na mfoori kulingana na vipimo na namna ya utengenezaji kwa maelezo sahihi kutoka kwa mtaalamu wa kilimo. Ikiwa mkulima atatumia viuatilifu, ni muhimu kutumia kulingana na ushauri wa wataalamu. Pia kuepuka kulima zao hili katika msimu ambao wadudu hao wanakuwepo kwa kasi hasa kipindi cha kiangazi.
Mavuno
Kwa wastani, bilinganya nyeupe hutoa kilogramu 10,000 hadi 15,000 kwa ekari moja. Aina hii ya bilinganya haina tofauti sana na aina nyingine kwani huchukua siku 80 hadi 95 kukomaa na kuanza kuvunwa. Kiwango cha mavuno huongezeka mchumo baada ya mchumo, kadri siku zinavyoendelea na pia kulingana na matunzo. Bilinganya hutoa mavuno mengi na bora kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo, baada ya hapo mavuno huwa hafifu.
Matumizi
Mboga hii hutumika kwa ajili ya kutengeneneza saladi japo wengine pia hutumia kama mboga au kama kiungo cha chakula.

Fursa kupitia technolojia ya kilimo cha Greenhouse



Karibu sana:

Kwanza tuanze kwa kupata tafsiri ya neno lenyewe, Greenhouse imekua ikipatiwa majina tofauti tofauti, wapo watu wanaiita Nyumba ya Kijani, wengine wanaiita Banda Kitalu n.k Vyovyote utakavyopenda kuiita teknolojia hii, cha muhimu ni kuelewa nini hasa maana yake.



Greenhouse(Banda Kitalu):  ni teknolojia ya kuipatia mimea mazingira mazuri ambayo yataisaidia mimea/mazao kumea vizuri na kua na uzao mkubwa, mimea hii inapandwa kwenye banda, au nyumba maalumu. Teknolojia hii inatumika hasa kuikinga mimea usiathiriwe na mazingira haribifu ya hali ya hewa.



Mazingira haribifu ni kama upepo mkali, baridi kali, mvua kubwa, au mvua za mawe, mionzi mikali ya jua, joto kali , wadudu pamoja na magonjwa. Hayo ndio mazingira ambayo teknolojia hii inaleta suluhisho, kuhakikisha mimea inastawi vizuri bila ya kuathiriwa na moja ya matatizo hayo yaliyotajwa.



Teknolojia hii ilivumbuliwa huko kwenye nchi baridi, zaidi ya karne moja na nusu (miaka 150) iliyopita. Nchi zilizopo ukanda wa baridi, mazao ya kitropiki (mazao yanayo pendelea joto) ilikua haiwezekani kabisa kulimwa maeneo hayo ya ukanda wa baridi. Ndipo hapo wazo la kuvumbua Greenhouse lilipoibuka.



Nchi hizi walianza kutumia teknolojia hii maana nyumba hii ya kijani ilikua ina uwezo wa kutunza joto, na hivyo wakaanza kulima mazao ya ukanda wa joto kama mbogamboga (nyanya, hoho) na matunda. Pamoja na teknolojia hii kuanza kitambo kidogo katika nchi zilizoendelea, lakini kwa upande wa nchi zinazoendelea bado teknolojia hii ni mpya kwa watu wengi.  Teknolojia hii pia inatumika katika nchi za joto, japo kuna utofauti  kati yake na  zile za nchi za ukanda wa baridi.



Faida za Greenhouse



  • Mavuno yanakua mara 10 hadi 12 zaidi ya kilimo cha eneo la wazi, ikitegemea aina ya mazao yanayolimwa humo, aina greenhouse pamoja na vifaa vya kudhibiti mazingira ya ndani ya greenhouse.
  • Uhakika wa kuvuna mazao unaongezeka. Maana Greenhouse inaweza kuzuia visababishi vya  uharibifu wa mazao.
  • Uzalishaji wa mazao katika kipindi chote cha  mwaka, maana huhitaji kusubiri mpaka msimu wa zao ufike ndio ulime.
  • Uwezo wa kupata soko zuri la mazao. Greenhouse itakuwezesha kuzalisha kipindi ambacho sio cha msimu (off- season) kwa vile kipindi hiki watu wengi hawazalishi kutokana na mazingira kutoruhusu,  ukiwa na greenhouse una uwezo wa kuzalisha kipindi hicho na ukapata bei nzuri
  • Ufanisi katika utumaji wa dawa, viwatilifu katika kudhibiti.
  • Matumizi ya maji ni madogo sana na udhibiti  wake  ni rahisi. Miundombinu ya umwagiliaji inayotumika hapa ni umwagiliaji wa matone (drip irrigation) ambapo maji yanakwenda pale penye mmea pekee.
  • Uwezo wa kutunza mimea inayozalishwa maabara kutokana na teknolojia ya tishu (tissue culture technology) mimea inapotoka maabara kabla haijapelekwa shambani inatunzwa kwanza kwenye greenhouse maalumu kwa ajili  ya kuzoea mazingira ya nje kwanza.
  • Uwezo wa kupanda mimea bila kutumia udongo (soilless culture).  Kutokana na changamoto ya magonjwa na vijidudu vya kwenye udongo kama Nematodes, ndipo uvumbuzi  wa teknolojia ya kupanda mimea kwa kutokutumia udongo ulipotokea



Baadhi ya Nchi zinazofanya vizuri kilimo cha  Greenhouse.
Kuna nchi zaidi ya 50 katika dunia ambapo kilimo kinalimwa kwenye greenhouse. Tutaangalia baadhi ya nchi ambazo zimekua zikifanya vizuri kupitia teknolojia hii. Tuanze na Marekani, Marekani ina eneo takribani 4000 hekta ambazo zina greenhouse kwa ajili ya kilimo cha maua,



Marekani kupitia kilimo hicho wanapata pato la zaidi ya Dola bilioni 2.8 (zaidi ya trilioni 5 hela za Tz) kwa mwaka. Nchini Hispania inakadiriwa zaidi 25,000hekta na Italia ni hekta 18,500, zimefungwa  greenhouse kwa kilimo cha pilipili hoho, strawberry, matango, maharagwe machanga,  pamoja na nyanya.



Canada greenhouse ni kwa kilimo cha maua na mboga mboga wakati ambapo hazilimwi kwingine. Mazao maarufu  yanayolimwa kwenye Greenhouse za Canada kama nyanya, matango na hoho.
Uholanzi ni zaidi ya hecta 89,600 zipo nchini ya greenhouse.



Uholanzi sekta ya greenhouse ndio iliyo bora zaidi duniani. Uholanzi ndio nchi inayoongoza kwa teknolojia hii na wamepiga hatua mbali sana. Yapo makampuni makubwa ya Kiholanzi yanayotumia teknolojia hii baadhi yao yapo hapa Tanzania katika kilimo cha maua, matunda, mbogamboga, pamoja na mbegu. Mfano : Kili Hortex, Multi flower, Mount Meru Flower, Enza Zaden, RJK ZWAAN (Q-SEM na AFRISEM)



Israel: 15000 hekta. Israel ndiyo nchi inayoongoza kwa kuuza maua (cut flowers) nje ya nchi. Japokuwa nchi ya Israel eneo lake kubwa ni jangwa. Pia Nchi ya Israel imekua moja ya nchi zilizopo mstari wa mbele katika teknolojia ya umwagiliaji na Greenhouse.



Balton Tanzania yenye makao yake makuu mjini Arusha, ni moja ya kampuni toka Israel zinazofanya vizuri katika sekta hii.



Uturuki: hekta 10,000 zinalimwa maua na mbogamboga kwa kutumia teknolojia hii ya Green house. Saudi Arabia: 90% ya mazao ya yanya na tango yanalimwa kwenye green house.



Misri 10,000 hekta nyanya, matango na pilipili hoho. Teknolojia ya Greenhouse nchini China inakua kwa kasi sana kuliko nchi yeyote   Japokuwa teknolojia hii haijaanza muda mrefu kivile huko China lakini mpaka sasa zaidi ya hekta 48,000 tayari zimefungwa Greenhouse.  Nchi nyingine zinzofanya vizuri barani Asia ni kama  Japan (40,000hekta) na Korea kusini (21,000 hekta).



Aina za Greenhouse.
Greenhouse zinagawanyika makundi mbalimbali kutegemeana na vigezo vifuatavyo:



Aina za Greenhouse kwa  kigezo cha sura/umbile (shape)
Zipo aina aina 8 za greenhouse, hapa nitataja chache tu kwa majina yake ya kitaalamu



  • Quonset Greenhouse
  • Saw tooth type
  • Even span type greenhouse
  • Uneven span type greenhouse



Aina za Greenhouse kwa kigezo cha Matumizi



  • Green house zinazoongeza joto (Hizi ni kwa maeneo ya baridi)
  • Greenhouse zinazopunguza joto (hizi ni kwa maeneo ya joto)



Aina za greenhouse kwa kigezo cha matengenezo yake (construction)



  • Greenhouse za miti (Wooden framed structure)
  • Pipe framed structure (Greenhouse zinazotumia mabomba)
  • Truss/Aluminium framed structure ( Geenhouse zinazojengwa kwa vyuma)



Aina za Greenhouse kwa kigezo  cha aina ya zana za ufunikaji (covering types)

  • Greenhouse zinazofunikwa kwa zana za Vioo (Glass Greenhouse or Screenhouse) )- hizi zinatumika sana maeneo ya baridi kali, ili kutunza joto kwa muda mrefu ndani   greenhouse
  • Greenhouse zinazofunikwa kwa mifuko ya plaski (plastic film)



Aina ya Greenhouse kwa kigezo cha uwekezaji unaofanywa:



  • Greenhouse za gharama kubwa (High cost greenhouse) ( Zaidi ya milioni 50)
  • Greenhouse za gharama za kati (medium cost greenhouse) (milioni 20 hadi 50)
  • Greenhouse za gharama ndogo (Low cost greenhouse) (chini ya milioni 20)
  • Greenhouse za gharama ndogo ndio watu wengi wanazitumia sana katika nchi zinazoendelea.

Teknolojia Katika Kilimo: Kilimo Cha Greenhouse Na Aina Zake



Habari  ndugu msomaji wetu, ni matumaini yangu unaendelea vizuri na mapambano ya kuelekea kwenye mafanikio.  Karibu tena katika kona hii ya kupata maarifa ya kilimo. Kutokana na maombi na maswali kadhaa ya watu kuhusu Kilimo cha Greenhouse, leo nitapenda tuanze kujifunza kuhusu mada hiyo ya Greenhouse. Leo tutaangazia kwanza maana ya teknolojia hiyo, historia yake, faida zake, Aina zake, pamoja na  mazao yanayolimwa kwenye Greenhouse

Karibu sana:
Kwanza tuanze kwa kupata tafsiri ya neno lenyewe, Greenhouse imekua ikipatiwa majina tofauti tofauti, wapo watu wanaiita Nyumba ya Kijani, wengine wanaiita Banda Kitalu n.k Vyovyote utakavyopenda kuiita teknolojia hii, cha muhimu ni kuelewa nini hasa maana yake.

Greenhouse(Banda Kitalu):  ni teknolojia ya kuipatia mimea mazingira mazuri ambayo yataisaidia mimea/mazao kumea vizuri na kua na uzao mkubwa, mimea hii inapandwa kwenye banda, au nyumba maalumu. Teknolojia hii inatumika hasa kuikinga mimea usiathiriwe na mazingira haribifu ya hali ya hewa. Mazingira haribifu ni kama upepo mkali, baridi kali, mvua kubwa, au mvua za mawe, mionzi mikali ya jua, joto kali , wadudu pamoja na magonjwa. Hayo ndio mazingira ambayo teknolojia hii inaleta suluhisho, kuhakikisha mimea inastawi vizuri bila ya kuathiriwa na moja ya matatizo hayo yaliyotajwa.

Teknolojia hii ilivumbuliwa huko kwenye nchi baridi, zaidi ya karne moja na nusu (miaka 150) iliyopita. Nchi zilizopo ukanda wa baridi, mazao ya kitropiki (mazao yanayo pendelea joto) ilikua haiwezekani kabisa kulimwa maeneo hayo ya ukanda wa baridi. Ndipo hapo wazo la kuvumbua Greenhouse lilipoibuka. Nchi hizi walianza kutumia teknolojia hii maana nyumba hii ya kijani ilikua ina uwezo wa kutunza joto, na hivyo wakaanza kulima mazao ya ukanda wa joto kama mbogamboga (nyanya, hoho) na matunda. Pamoja na teknolojia hii kuanza kitambo kidogo katika nchi zilizoendelea, lakini kwa upande wa nchi zinazoendelea bado teknolojia hii ni mpya kwa watu wengi.  Teknolojia hii pia inatumika katika nchi za joto, japo kuna utofauti  kati yake na  zile za nchi za ukanda wa baridi.


Faida za Greenhouse

Mavuno yanakua mara 10 hadi 12 zaidi ya kilimo cha eneo la wazi, ikitegemea aina ya mazao yanayolimwa humo, aina greenhouse pamoja na vifaa vya kudhibiti mazingira ya ndani ya greenhouse.
Uhakika wa kuvuna mazao unaongezeka. Maana Greenhouse inaweza kuzuia visababishi vya  uharibifu wa mazao.
Uzalishaji wa mazao katika kipindi chote cha  mwaka, maana huhitaji kusubiri mpaka msimu wa zao ufike ndio ulime.
Uwezo wa kuzalisha kipindi ambacho sio cha msimu (off- season) kwa vile kipindi hiki watu wengi hawazalishi kutokana na mazingira kutoruhusu,  ukiwa na greenhouse una uwezo wa kuzalisha kipindi hicho na ukapata bei ya juu na
Ufanisi katika utumaji wa dawa, viwatilifu katika kudhibiti.
Matumizi ya maji ni madogo sana na udhibiti  wake  ni rahisi. Miundombinu ya umwagiliaji inayotumika hapa ni umwagiliaji wa matone (drip irrigation) ambapo maji yanakwenda pale penye mmea pekee.
Uwezo wa kutunza mimea inayozalishwa maabara kutokana na teknolojia ya tishu (tissue culture technology) mimea inapotoka maabara kabla haijapelekwa shambani inatunzwa kwanza kwenye greenhouse maalumu kwa ajili  ya kuzoea mazingira ya nje kwanza.
Uwezo wa kupanda mimea bila kutumia udongo (soilless culture).  Kutokana na changamoto ya magonjwa na vijidudu vya kwenye udongo kama Nematodes, ndipo uvumbuzi  wa teknolojia ya kupanda mimea kwa kutokutumia udongo ulipotokea


Baadhi ya Nchi zinazofanya vizuri kilimo cha  Greenhouse.
Kuna nchi zaidi ya 50 katika dunia ambapo kilimo kinalimwa kwenye greenhouse. Tutaangalia baadhi ya nchi ambazo zimekua zikifanya vizuri kupitia teknolojia hii. Tuanze na Marekani, Marekani  ina eneo takribani 4000 hekta ambazo zina greenhouse kwa ajili ya kilimo cha maua, Marekani kupitia kilimo hicho wanapata pato la zaidi ya Dola bilioni 2.8 (zaidi ya trilioni 5 hela za Tz) kwa mwaka. Nchini Hispania inakadiriwa zaidi 25,000hekta na Italia ni hekta 18,500, zimefungwa  greenhouse kwa kilimo cha pilipili hoho, strawberry, matango, maharagwe machanga,  pamoja na nyanya. Canada greenhouse ni kwa kilimo cha maua na mboga mboga wakati ambapo  hazilimwi kwingine. Mazao maarufu  yanayolimwa kwenye Greenhouse za Canada kama nyanya, matango na hoho.

Uholanzi ni zaidi ya hecta 89,600 zipo nchini ya greenhouse. Uholanzi sekta ya greenhouse ndio iliyo bora zaidi duniani. Uholanzi ndio nchi inayoongoza kwa  teknolojia hii na wamepiga hatua mbali sana. Yapo makampuni makubwa ya Kiholanzi yanayotumia teknolojia hii baadhi yao yapo hapa Tanzania katika kilimo cha maua, matunda, mbogamboga, pamoja na mbegu. Mfano : Kili Hortex, Multi flower, Mount Meru Flower, Enza Zaden, RJK ZWAAN (Q-SEM na AFRISEM)

Israel: 15000 hekta. Israel ndiyo nchi inayoongoza kwa kuuza maua (cut flowers) nje ya nchi. Japokuwa  nchi ya Israel eneo lake ni kubwa ni jangwa. Pia Nchi ya Israel imekua moja ya nchi zilizopo mstari wa mbele katika teknolojia ya umwagiliaji na Greenhouse. Balton Tanzania yenye makao yake makuu mjini Arusha, ni moja ya kampuni toka Israel zinazofanya vizuri katika sekta hii.

Uturuki: hekta 10,000 zinalimwa maua na mbogamboga kwa kutumia teknolojia hii ya Green house. Saudi Arabia: 90% ya mazao yanya na tango yanalimwa kwenye green house. Misri  10,000 hekta nyanya, matango na pilipili hoho. Teknolojia ya Greenhouse nchini China inakua kwa kasi sana kuliko nchi yeyote  duniani. Japokuwa teknolojia hii haijaanza muda mrefu kivile huko China lakini mpaka sasa zaidi ya hekta 48,000 tayari zimefungwa Greenhouse.  Nchi nyingine zinzofanya vizuri barani Asia ni kama  Japan (40,000hekta) na Korea kusini (21,000 hekta).

Aina za Greenhouse.
Greenhouse zinagawanyika makundi mbalimbali kutegemeana na vigezo vifuatavyo:

1.  Aina za Greenhouse kwa  kigezo cha sura/umbile (shape)
Zipo aina aina 8 za greenhouse, hapa nitataja chache tu kwa majina yake ya kitaalamu
Quonset Greenhouse
Saw tooth type
Even span type greenhouse
Uneven span type greenhouse
2. Aina za Greenhouse kwa kigezo cha Matumizi
Green house zinazoongeza joto (Hizi ni kwa maeneo ya baridi)
Greenhouse zinazopunguza joto (hizi ni kwa maeneo ya joto)
3. Aina za greenhouse kwa kigezo cha matengenezo yake (construction)
Greenhouse za miti (Wooden framed structure)
Pipe framed structure (Greenhouse zinazotumia mabomba)
Truss/Aluminium framed structure ( Geenhouse zinazojengwa kwa vyuma
4. Aina za Greenhouse kwa kigezo  aina ya zana za ufunikaji (covering types)
Greenhouse zinazofunikwa kwa  zana za Vioo (glass)- hizi zinatumika sana maeneo ya baridi kali, ili kutunza joto kwa muda mrefu ndani   greenhouse
Greenhouse zinazofunikwa kwa mifuko ya plaski (plastic film)
5. Aina ya Greenhouse kwa kigezo cha uwekezaji unaofanywa
Greenhouse za gharama kubwa (High cost greenhouse) ( Zaidi ya milioni 50)
Greenhouse za gharama za kati (medium cost greenhouse) (milioni 20 hadi 50)
Greenhouse za gharama ndogo (Low cost greenhouse) (chini ya milioni 20)

Kilimo cha Matango



Ni zao linalopendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°C
Udongo Hustawi vizuri katika udongo tifutifu wenye rutuba usiotuamisha maji
Maandalizi ya shamba Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30 hadi 45

Weka matuta ya mwinuko yenye upana wa mita 1 hadi 1.5 kutoka kati ya tuta na tuta
Upandaji Zipo aina mbili za upandaji,

1.ya kwanza ni ile ya kupanda mbegu moja kwa moja na
2. ya pili ni ile ya kupanda mbegu katika trei na kuhamisha baada ya siku 8 hadi 10.
Njia ya kupanda mbegu moja kwa moja ni rahisi lakini ile ya kupanda katika trei ni bora zaidi kwani shamba hujaa vizuri katika nafasi na hukua haraka na kuzaa mavuno mengi.

Pima mashimo ya kupandia katika umbali wa sentimita 20 hadi 25 kutoka shina hadi shina mstari mmoja kwa tuta na sentimita 40 katika mfumo wa zig-zag pande zote mbili za tuta na kupanda
Mbolea kianzio iwekwe katika kila shimo na kupanda endapo miche kutoka katika trei itatumika Hakikisha shamba lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda.




Palizi Palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu Magugu hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya viuagugu.

Njia nyingine ni matumizi ya plastiki maalum kuzuia magugu yaani ‘plastic mulch’
Mbolea Tumia mbolea ya DAP wakati wa kupanda na kisha tumia NPK yenye uwiano mmoja kama, 18:18:18, 17:17:17 ama 16:16:16 baada ya wiki tatu toka Usegekaji.

Tumia nguzo za unene wa inchi 2 na kamba ili kuinua mimea na matunda yasiguse ardhi na kuoza
Uchavushaji.

Hii ni muhimu sana kuzingatiwa kwani tango huchavushwa kwa wadudu na si upepo
.Bila wadudu kama nyuki uzalishaji huathrika sana.

Ni muhimu kupanda mazao kama alizeti na maua mbali mbali yanayopendwa na wadudu wachavushaji ili kuhakikisha uwepo wa wadudu hao shambani.


Aidha inapo-lazimu ni vema kuweka mizinga kadhaa ya nyuki katika shamba la tango
Matumizi ya viuatilifu Katika udhibiti wa wadudu na magonjwa matumizi ya viuatilifu yafanyike kwa maelekezo ya wataalam.

kubaini tatizo na kiuatilifu hitajika na namna ya matumizi yake
Mavuno Mavuno huanza baada ya siku 40 hadi 45 kutegemea na aina pamoja na hali ya hewa...

Kilimo Bora cha Nyanya


Utangulizi

Nyanya ni zao la mboga linalolimwa sehemu nyingi duniani kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara. Nyanya ni aina ya mboga inayo zalishwa kwa wingi sana duniani. Kwa Tanzania, nyanya ni zao la kwanza katika mazao ya mboga linalolimwa na kuliwa kwa wingi ukilinganisha na mboga zingine. Nyanya hutumika karibu katika kila mlo. Kulingana na umuhimu wa zao hili kama chakula na pia kama zao linalomwingizia kipato mkulima, kuna haja ya kutoa mafunzo kuhusu mbinu bora za uzalishaji wake.

Maeneo yanayolima nyanya

Inadhaniwa kuwa asili ya nyanya ni nchi ya Peru au Equador huko Amerika ya Kusini. Mmea huu ulianza kuzalishwa kama zao katika nchi ya Mexico na baadaye kusambaa katika nchi nyingine za ulimwengu.

Nchi zinazolima nyanya kwa wingi duniani ni pamoja na USA, Italia na Mexico. Kwa upande wa Africa ni kama; Malawi, Zambia na Botswana. Zao hili hulimwa pia katika nchi za Africa Mashariki, ikiwemo Kenya, uganda na Tanzania.
Kwa upande wa Tanzania mikoa inayolima nyanya kwa wingi hasa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na biashara ni pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro (Hai, Moshi na Rombo), Arusha (Arumeru), Morogoro (Mgeta), Iringa (Ilula), Tanga (Lushoto), Mbeya (Mbeya vijijini) na Singida.



Mazingira yanayofaa kwa kilimo cha nyanya

Hali ya Hewa: Nyanya hustawi vizuri zaidi kwenye mazingira ya joto la wastani kuanzia nyuzi joto 18-27 sentigreti. Mvua nyingi husababisha mlipuko wa magonjwa ya ukungu kama vile Baka jani chelewa)

Udongo: Nyanya hustawi kwenye aina zote za udongo kuanzia udongo wa kichanga, mweupe wa tifutifu hadi udongo wa mfinyanzi, ili mradi uwe na mboji ya kutosha na usiosimamisha/tuamisha maji. Pia uwe na uchachu wa wastani yaani pH 6.0 - 7.0.

Mwinuko: Nyanya hustawi vizuri kutoka sehemu za mwambao hadi kwenye mwinuko wa mita 400-1500 kutoka usawa wa bahari; yaani nyanda za chini kati hadi za juu kutoka usawa wa bahari. Nyanya zinazopandwa nyanda za juu sana hukumbwa na mvua za mara kwa mara ambazo huambatana na magonjwa ya jamii ya ukungu; kama Bakajani chelewa (Late Blight)

Aina za nyanya

Kutokana na tabia ya ukuaji, nyanya zinagawanyika katika makundi mawili:
  1. Aina ndefu (intermediate) kwa mfano ANNA F1, Tengeru 97, Marglobe (M2009). Aina hizi hufanya vizuri zaidi zinapopandwa ndani ya greenhouse. Uvunaji wake ni wa muda mrefu, zipo ambazo zinavunwa hata zaidi ya miezi 6, yaani hiyo miezi 6 ni ya uvunaji.
  2. Aina fupi (determinate) kwa mfano Tanya, Cal J, Mwanga, Onyx, Roma VF (nyanya mshumaa)
Kulingana na uchavushaji, nyanya zinagawanyika katika makundi mawaili:
  1. OPV (Open Pollinated Variety) - Hizi ni aina za kawaida
  2. Hybrid - Chotara: Hizi ni nyanya zilizoboreshwa, aina hii zina mavuno mengi, kati ya hizo zipo aina fupi na ndefu.

Hata hivyo katika karne hii ya 21, nyanya zinazopendelewa kulimwa zaidi na wakulima, ni zile zinazoweza kuvumilia magonjwa, zinazo zaa sana, na zenye ganda gumu ili kufanikisha usafirishaji, na kuhifadhika kwa siku nyingi bila kuharibika mapema. Nyanya zinazoonyesha kuwa na sifa ya kuhifadhika bila kuharibika mapema ni kama:
a) Tengeru’97 ambayo ina sifa vifuatazo:
  • Huzaa sana kutokana na wingi wa matunda na muda mrefu wa kuvuna, ambao hufikia michumo mikubwa kati ya 6-7 kuanzia kuvuna hadi mwisho wa mavuno.
  • Aina hii ina sifa ya kuwa na ganda gumu, hivyo haziharibiki haraka wakati wa kusafirisha au kuhifadhi (wastani wa siku 20)
  • Zina sifa ya kuvumilia baadhi ya magonjwa kama vile ugonjwa wa kunyauka
  • Tengeru’97 hustahimili mashambulizi ya minyoo fundo (Root knot nematodes)
b) Tanya
  • Sifa kubwa ya Tanya ni kwamba nayo huzaa sana
  • Huwa na ganda/ngozi ngumu ambayo inazuia kuoza au kuharibika kwa urahisi wakati wa kusafirisha au wakati wa kuhifadhi kwa muda mrefu.
  • Tanya nayo ina ladha nzuri inayopendelewa na walaji wengi

Zingatia: Tatizo la Tanya na T97 ni kwamba si kubwa sana kama marglobe 2009. Lakini ukubwa ni karibu unge karibiana, haujapishana sana. Kwa ujumla, ukubwa na wingi wa mazao hutegemea sana matunzo, udongo, hali ya hewa na mazingira kwa ujumla.

Maandalizi ya Shamba la Nyanya

Shamba la nyanya liandaliwe mwezi mmoja au miwili kabla ya kupanda miche. Mara baada ya kulima choma nyasi juu ya udongo au ondoa magugu yote yanayoweza kuhifadhi wadudu na magonjwa ya nyanya. Siku moja au mbili kabla ya kuhamishia nyanya shambani, mwagilia sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuhamishia nyanya. Andaa mashimo ya nyanya kutegemeana na idadi ya miche uliyonayo, nafasi na aina ya nyanya. Nafasi kati ya mche hadi mche ni wastani wa sentimita (50-60) x (50-75) kutegemeana na aina au zao litakalo changanywa na nyanya.

Jinsi ya kupanda miche ya nyanya

Weka samadi viganja viwili au gram 5 za mbolea ya kupandia kwenye shimo kabla ya kupanda mche.

Hamisha miche toka kitaluni pamoja na udongo wake
Sambaza mizizi vizuri kwenye shimo bila kukunja.
Fukia miche kina kile kile ambacho shina lilikuwa limefukiwa kitaluni.
Mwagilia maji ya kutosha kulingana na unyevunyevu uliopo kwenye udongo kisha weka matandazo na kivuli ili kupunguza uharibifu unaosababishwa na mionzi ya jua.

Utunzaji wa zao la nyanya shambani

Umwagiliaji wa nyanya
Nyanya, kama ilivyo kwa mazao mengine, zinahitaji maji mengi ili kuzaa matunda yenye afya. Kutegemeana na aina ya udongo, unaweza kumwagilia nyanya mara mbili kwa wiki. Hakikisha unapanga ratiba maalum ya kumwagilia na unaifuata ili kuepuka kumwagilia kiholela holela kwani umwagiliaji usio na mpangilio huathiri afya ya matunda ya nyanya na kupelekea nyanya kuoza kitako (tomato blossom end rot). Unapotumia vifaa kama water can au mpira jitahidi sana usimwagilie kwenye majani ya mmea au matunda kwa sababu kulowesha mmea kunavutia wadudu na magonjwa ya ukungu unaoharibu nyanya.

Zingatia: usituamishe maji kwenye bustani au shamba la nyanya,

Palizi: Kudhibiti magugu
Hakikisha shamba ni safi wakati wote, palilia shamba na hakikisha magugu yote hasa yale ya jamii ya nyanya yamelimiwa chini. Palilia shamba lako wiki ya pili au ya tatu baada ya kupandikiza miche, lakini unaweza kupalilia kila unapoona magugu kwani shamba linatakiwa kuwa safi muda wote. Unaweza kuondoa magugu kwa kutumia dawa za kuua magugu au jembe la mkono. Magugu ni hatari kwa sababu tatu:

Kwanza: magugu yanashandana na mimea katika kuchukua nafasi na hivyo mimea kushindwa kujitanua. Pili: magugu huzuia mimea ya nyanya kupata mwanga wa jua wakutosha hivyo kuifanya mimea kushindwa kujitengenea chakula cha kutosha. Na tatu: magugu hushindana na mimea ya nyanya kufyonza virutubisho/chakula ardhini kitu ambacho kinapelekea mimea kuwa dhaifu. Pia magugu yanahifadhi wadudu na magonjwa na hivyo kuhatarisha zaidi usalama wa nyanya.

Mahitaji ya mbolea kwenye nyanya
Mbolea ya kupandia: weka mbolea ya DAP au Minjingu wakati wa kupandikiza miche shambani. Kiasi cha gram 5 ambayo ni sawa sawa na kifuniko kimoja cha soda kinatosha kwa kila shimo lenye mche mmoja. Tanguliza mbolea kwanza kwenye shimo kisha funika na udongo kiasi ili mbolea isigusane moja kwa moja na mizizi ya nyanya.

Mbolea ya kukuzia: unatakiwa kuongeza mbolea ya kukuzia kipindi cha wiki mbili au tatu baada ya kupandikiza miche shambani. Mbolea hii ya iwekwe kuzunguka shina la mmea kwa umbali wa sentimeta 5 kutoka kwenye shina. Kwa ajili ya kukuzia mimea ya nyanya tumia mbolea kama vile CAN, NPK, au SA. Tumia kifuniko kimoja cha soda kwa shina. Mbolea hii inaweza kuwekwa mara mbili kabla ya mvuno wa kwanza.


Ili kurefusha kupindi cha uzaaji wa zao la nyanya (na hata mazao mengine yatoayo matunda kama vile nyanya chungu, biringanya, na pilipili hoho) inapaswa kuongezea mbolea katika kipindi cha uvunaji mfano baada ya kuvuna mara mbili unashauriwa kuongeza mbolea ya samadi na mbolea kama vile NPK. Hii inasaidia mmea kuendelea kutoa maua bila kuchoka.

Kwa kawaida nyanya fupi jamii ya “Roma” huweza kuzaa na kuvunwa kwa kipindi cha wiki 6 hadi 8 tu. Lakini kama utakuwa unaongezea mbolea na kukazania matunzo ya shambani (hasa usafi wa shamba na kumwagilia maji ya kutosha), nyanya zinaweza kuendelea kuzaa kwa muda mrefu zaidi. Hii ni tofauti na mazoea ya wakulima wengi kuwa mara nyanya zianzapo kuzaa huduma za palizi na usafi wa shamba huachwa na kutilia maanani kazi ya kuvuna pekee. Hii inajitokeza zaidi kwenye aina ya nyanya fupi.

Kuweka matandazo
Matandazo ni nylon, majani au takataka za mimea zinazowekwa shambani au bustanini kwa lengo la kutunza unyevu na kuzuia au kupunguza kasi ya uotaji wa magugu, pia yakioza huongeza rutuba kwenye udongo. Mfano wa matandazo yanayoweza kutumika katika shamba la nyanya ni: nylon/turubai (plastic mulch), majani makavu, majani ya migomba, pumba za mazao, takataka za mbao. Plastic mulch inawekwa kabla ya kupandikiza miche shambani lakini matandazo mengine yawekwe baada ya kupandikiza miche. Na inafaa yawekwe kuzunguka eneo la shimo la mmea au katika shamba zima. Hivyo ni vizuri matandazo ya aina hii yawekwe mara tu baada ya kupandikiza (kama shamba halina magugu) au baada ya palizi ya kwanza.

Kupogolea matawi

Punguza matawi na vikonyo ili kuongeza mwanga wa kutosha kwenye nyanya pamoja na kuruhusu mzunguko wa kutosha wa upepo na kusababisha mazingira magumu ya wadudu maadui kwenye nyanya, hasa wale wanaopenda kiza na magonjwa yanayopendelea unyevunyevu.

Kwa nyanya fupi ni vizuri kuhakikisha kuna matawi mengi iwezekanavyo ili kuweza kupata matunda mengi zaidi. Hivyo usipunguze matawi katika aina hii ya nyanya. Kwa nyanya ndefu zenye kuhitaji uegemezi, unashauriwa kukuza nyanya kwa tawi moja lisilo na vichipukizi pembeni au matawi mawili na kuacha mnyanya urefuke.

Kupogolea majani
Kupunguza majani ni muhimu pia katika kupunguza maambukizo ya ukungu katika shina na pia kutoa nafasi ili mwanga kupenya na kuruhusu mzunguko wa hewa. Kwa nyanya ndefu, majani ya chini ya matunda huondolewa kadiri unavyo endelea kuvuna.

Majani yapunguzwe kipindi cha asubuhi kwa kutumia mkono na siyo kisu kwani kinaweza kueneza magonjwa kutoka mche hadi mche. Ondoa majani yote ambayo yana dalili za magonjwa, yaliyozeeka, yaliyobadilika rangi na kuwa njano au kuanza kukauka. Wakati wa utoaji majani kuwa makini kutojeruhi shina kwani maambukizi yanaweza kuanzia hapo.

Kumbuka: Matawi/majani ya chini ya mmea wowote huwa hayana msaada sana katika uzaaji wa matunda na zaidi ni kwamba kwa kiasi kikubwa yamepoteza uwezo wake wa kutengeneza chakula. Hivyo kuendelea kubaki kwake kutapunguza chakula ambacho kingeenda kuongeza wingi na kukuza ukubwa wa matunda.

Kusimikia miti (staking)
Nyanya ziwekewe miti/mambo ili kuzuia zisianguke au kutambaa kwenye udongo, jambo ambalo linaweza kusababisha madhara mengi ya nyanya. Nyanya zinazotambaa zinahitaji kusaidiwa kuonyeshwa njia ili zisiguse chini. Nyanya zinapotambaa ardhini au kugusa chini zinaweza kuambukizwa wadudu na magonjwa ya ardhini kwa urahisi sana na pia wakati wa jua kali nyanya huchomwa na joto kali la ardhini. Hivyo basi shindilia mti mmoja (pigilia chini mambo) kando ya kila mmea wa nyanya na tumia kamba kufunga shina la mmea kwenye mti huo. Simika miti wiki mbili baada ya kupandikiza miche. Miti iwe imara na isiyooza haraka. Iwe na urefu wa mita moja hadi mbili na unene usiopungua sm 2.

Uvunaji wa nyanya

Vuna wakati nyanya zimekomaa lakini bado zina rangi ya kijani. Wakati wa kuvuna nyanya tenganisha tunda na kikonyo chake na sio kikonyo na shina ili kuepuka kuujeruhi mmea kitu ambacho kinaweza hurahisisha maambikizi ya magonjwa kwa mimea. Wakati mzuri wa kuvuna ni asubuhi na jioni. Inatakiwa nyanya ziwekwe kwenye vyombo vinavyopitisha hewa, na vyombo maarufu ni matenga. Matenga ya nyanya yanaweza kuwa yametengenezwa kwa mbao au mianzi.

Mara tu baada ya kuvuna/kuchuma nyanya inashauriwa zikusanywe chini ya kivuli kwa muda ili ziweze kutoa joto la shambani kabla ya kuzifungasha kwenye matenga.

Namna ya kuhifadhi nyanya

Nyanya ni miongoni mwa mazao mepesi sana kuharibika hivyo ni muhimu sana nyanya zihifadhiwe mahali ambapo hapataharakisha kuoza kwake. Mahali pazuri ni pale penye ubaridi kiasi. Nyanya zenye ukijani zinaweza kuhifadhiwa mahali penye joto la 8o C hadi 10o C na zinaweza kukaa kwa muda wa hadi wiki tano bila kuharibika. Nyanya zilizoiva zinaweza kuhifadhiwa mahali penye kiasi cha joto cha 7o C na ni vizuri zaidi kama zitauzwa au kutumika mapema, yaani isizidi wiki moja. Katika mahali pakuhifadhia nyanya hali ya unyevu anga inatakiwa iwe ni kati ya 85% hadi 90%.

Hivi ndivyo tunavyohitimisha makala hii ya kilimo bora cha nyanya


UJENZI WA BANDA LA KUKU

Ujenzi wa mabanda bora ya kuku ni miongoni mwa mambo ya msingi kabisa katika ufugaji bora wa kuku wawe ni wa asili au wale walioboreshw...